
KUHUSU SISI
Ahlu Sunna Wal Jamaa Hajj and Umra Trust ni taasisi ya kidini inayopatikana Zanzibar, Pemba na Dar es Salaam. Taasisi hii inawawezesha na kuwarahisishia mahujaji kwenda Saudia Arabia (Makka na Madina) kwa ajili ya Hijja na Umra kila mwaka. Tunajivunia uzoefu wa zaidi ya miaka 13 sasa, ubora na uhakika wa huduma zetu.
DHAMIRA YETU
Sisi, taasisi ya Ahlu Sunna Wal Jamaa Hajj and Umra Trust tunakuhakikishia unafanya ibada za Hijja na Umra kila mwaka bila changamoto zozote kama vile malazi, ibada na afya, huku ukifurahia ziara kwenye maeneo matakatifu na ya kihistoria.

KWA NINI UTUCHAGUE SISI
Taasisi yetu imekuwa na huduma bora inayoendelea kukua kila mwaka, ubora wa uendeshaji huduma, timu ya wataalam, upatikanaji wa msaada wakati wote, matokeo bora ya kuridhishwa kwa huduma kutoka kwa wateja wetu na utayari wa kukusikiliza na kukushauri inapohitajika.